Rais Magufuli awawasili nchini akitokea nchini Rwanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amewasili nchini akitokea nchini Rwanda ambapo alikuwa na ziara ya kikazi ya siku mbili.
Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini DSM, Rais Dkt Magufuli amepokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, Wakuu wa Wilaya za Temeke na Ilala pamoja na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Katika siku yake ya kwanza ya ziara nchini Rwanda Rais Magufuli pamoja na mwenyeji wake Rais wa Rwanda Paul Kagame walifungua daraja la kimataifa la Rusumo lililopo mpakani mwa Tanzania na Rwanda pamoja na kituo cha pamoja cha forodha.
Leo Alhamisi Aprili 7 Rais Magufuli pamoja na mke wake mama Janeth Magufuli wameungana na wananchi wa nchi hiyo ya Rwanda kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 22 tangu kutokea kwa mauaji ya kimbari yaliyosababisha vifo vya watu takriban milioni moja.
Kurejea kwake nchini kunahitimisha ziara yake ya kwanza kuifanya nje ya nchi aingie madarakani mwezi oktoba mwaka 2015.
0 comments:
Post a Comment