Madaktari wa Hosipitali Teule ya wilaya ya Arusha wameiomba serikali kushughulikia matatizo ya uhaba na uchakavu wa miundombinu unaoikabili hosipitali hiyo ili kupunguza mzigo wa lawama,malalamiko,na tuhuma wanazopata kutoka kwa wagonjwa.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dr.Josephat Kivuyo amemweleza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daud Ntebenda aliyewatembelea kuwa licha ya jitihada zinazofanyika kuboresha huduma,wananchi wamekuwa wakiwatazama kama wao ndio wanaosababisha mapungufu yaliyopo jambo linalowakatisha tamaa.
Aidha Dk.Kivuyo pamoja na kueleza matatizo mengi yanayohitaji kushughulikiwa katika hosipitali hiyo amesema kubwa linalohitaji kupewa kipaumbele ni pamoja na Sehemu ya upasuaji na kuboresha miundombinu ikiwemo ya maji.
Akizungumzia malalamiko hayo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw.Daud Ntebenda amesema serikali imeshaanza kushughulikia mapungufu yote katika hosipitali,zahanati na vituo vya afya na licha ya kuwaomba watendaji hao kuendelea kuwa wavumilivu amewataka wadau wa maendeleo kutoa ushirikiano.
hosipitali hiyo teule inategemewa na watu zaidi ya elfu sabini ambao wanapokosa huduma za msingi wote hukimbilia katika hosipitali ya mkoa wa arusha ya mount ambayo pia inakabiliwa na changamoto nyingi.
Home
Afya
Slider
Madaktari waiomba Serikali kushughulikia uchakavu wa miondombinu Hospitali ya wilaya ya Arusha.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment