Kungo wa Yanga,Thabani Kamusoko akimtoka kiungo wa Al Ahly, Hossan Ghaly(Picha na BinZubeir).
Na.Sadick Msangi,Dar es Salaam.
Mabingwa wa Tanzania bara timu ya soka ya Yanga imeshindwa kufurukuta mbele ya wamisri baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na al ahly ya misri katika mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika raundi ya 16 bora uliochezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga imeshindwa kutumia vema faida ya kucheza katika uwanja wake wa nyumbani mbele ya mashabiki wake baada ya kujikuta ikiruhusu goli la mapema katika dakika ya 10 likifungwa na straika matata amri Gamal kwa kichwa kufuatia mpira wa adhabu ndogo uliopigwa nje kidogo ya eneo la hatari.
Baada ya bao hilo yanga ilijaribu kutulia kwa kupanga mashambulizi kupitia mawinga wake Deus Kaseke na Issofou Boubakari na kufanikiwa kusawazisha bao hilo baada ya beki mmoja wa Al Ahly kujifunga akiwa katika jitihada za kuokoa krosi iliyopigwa na Issofou Boubakary.
Matokeo hayo yanaiweka yanga katika nafasi finyu ya kufuzu hatua inayofuata ya michuano hiyo kwani italazimika kupata ushindi wa idadi yoyote ya mabao au sare ya kuanzia magoli 2-2 katika mchezo wa maruadiano unaotarajia kuchezwa april 19 nchini misri.
Baada ya yanga kubanwa mbavu katika uwanja wa nyumbani sasa kesho Jumapili katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi saa 9 kamili alasiri, Azam FC watakua wenyeji wa Esperance Sportive de Tunis (EST) ya Tunisa katika mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) hatua ya 16 bora.
Waamuzi wa mchezo huo namba 75 ni Daniel Frazer Bennet, akisaidiwa na Zakhele Siwela, Thembisile Theophilus, mwamuzi wa akiba Mbongiseni Fakudze wote kutoka nchini Afrika Kusini, huku kamisaa wa mchezo akiwani Joseph Nkole kutoka nchini Zambia.
Home
MICHEZO
Slider
Yanga yabanwa mbavu kwa kulazimishwa sare ya 1-1 na Al Ahly Taifa Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment