Image
Image

Wajawazito watozwa gharama za dawa,kitanda na usajili wa Faili Hospitali ya Mkoa ya Lindi Sokoine.

Wakati Serikali ikijitahidi kuweka matangazo kila kona ya Hospitali mbalimbali za mikoa na vituo vya afya na huduma ya kujifungua kwa mama mjamzito ikiwa ni bure mambo yamebadilika kwenye Hospitali ya Mkoa ya Lindi Sokoine,ambapo wakina mama wajawazito wanalazimika kulipia gharama ya kitanda na usajili wa faili mara baada ya kujifungua,jambo ambalo wamelilalamikia na kuiomba serikali kuziondoa gharama hizo ili azma ya huduma hiyo iweze kufikiwa.
Baadhi ya wakina mama wamesema hawaoni maana ya huduma hiyo kuwa bure ili hali wanalipishwa,gharama za kitanda,shilingi elfu tano,usajili wa faili shilingi elfu tano na gharama za madawa pale yanapoitajika.
Kufuatia hali hiyo wameiomba serikali kuboresha zaidi huduma hiyo ili malengo ya kutoa huduma bure kwa wakina mama wajawazito liweze kufikiwa.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa ya Sokoine  Farida Ally amesema hana taarifa sahihi iwapo wakina mama hao wanatozwa gharama ya kitanda na usajili wa faili, huku akikiri wakina mama kununua dawa iwapo dawa walizoandikiwa hazipo hospitalini hapo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment