Image
Image

Rais Shein atangaza Serikali mpya isiyo ya mfumo wa umoja wa kitaifa ya Mawaziri 13 Manaibu 7.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali viliko Zanzibar wakati wa kutangaza Baraza lake Jipya la Mawaziri Ikulu.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza nao katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo asubuhi.
Mwandishi wa habari wa ITV na Redio One Farouk Karim alipata fursa ya kuuliza swali kwa Rais wa Zanzibar wakati wa mkutano huo na waandishi uliofanyika Ikulu Zanzibar leo.
Mwandishi wa habari wa Kituo cha TV cha Chanel Ten Munir Zakari akiuliza swali katika mkutano huo na Rais wa Zanzibar Dk Shein Ikulu Zanzibar.
Mwandishi wa Gazeti la Zanzibar Leo Ndg Hafsa Golo akiuliza swali kwa Rais wa Zanzibar wakati wa mkutano huo na waandishi wa kutangaza Baraza la Mawaziri Zanzibar.
 Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein ametangaza Serikali yake mpya isiyo ya mfumo wa umoja wa kitaifa ya mawaziri 13 huku akiwapa uwaziri na ujumbe wa Baraza la Mapinduzi Wapinzani.
Dr.Shein akizumgumza Ikulu ya Zanzibar mara baada ya kuitangaza Serikali hiyo yenye mawaziri 13 badala ya 17 ya awamu iliyopita na manaibu saba Dr.Shein amesema Serikali yake hyo ina  wapinzani kutoka chama cha ADC ambapo Mh.Hamad Rashid amekuwa waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi na Mh.Saidi Soud wa chama cha AFP na Juma Ali Khatibu wa TADEA ambao wanakuwa mawaziri wasiokuwa na wizara maalum lakini ni wajumbe wa Baraza la Mawaziri ni Serikali ya wananchi na ya mapinduzi.
Katika uteuzi huo Rais Shein amewarejesha mawaziri watatu wa awamu iliyopita Haroun Ali Suleiman-Katiba na Sheria, Haji Omar Kheri Tawala za Mikoa na Mohmaed Aboud Waziri wa Nchi na kuwatema wazamani wakiwemo Dr.Mwinyi Haji Makame, Omar Yussuf.
Dr.Shein pia amewateua manaibu waziri saba wote wapya wa afya,kilimo,habari,ujenzi,elimu,ardhi na katiba na sheria  tofauti na awamu iliyopita walikuwa wanane.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment