Madereva wa Daladala zinazofanya safari zake
kutoka Mjini kati naMkuzo,Mwengemshindo Mjini Songea wamegoma kwa siku moja
kutokana na ubovu wa barabara na kuamua kutengeneza barabara ya Mkuzo-Mauki
ambayo ni mbovu na hivyo wameiomba serikali
kuitengeneza barabara hiyo.
Wakitengeneza barabara hiyo kwa kushirikiana na makondakta wao pamoja
na madereva wa bodaboada wamesema kuwa
wameamua kusitisha usafiri wa daladala kwa muda
kutokana na ubovu wa barabara unaosababisha magari yao kuharibika na
hivyo wameamua kuitengeneza wao wenyewe.
Kwa upande wao wananchi wamezungumzua wakati mgumu
waliokutana nao kutokana na ubovu huyo wa barabara.
Kwa upande wake
mhandisi wa barabara wa manispaa ya songea Godfrey Majuto anasema kuwa
wametenga shilingi milioni kumi
na sita kurekebisha barabara hiyo
itakapopungua mvua wakati wakisubiri bajeti ya mwaka 2016/2017 na kwamba hakuna mpango wa kuitengeneza barabara hiyo
kwa kiwango cha lami kwa sasa.


0 comments:
Post a Comment