Madereva hao mapema jana wakati walipogoma walisema
kuwa kunyanyaswa huko na moja ya afisa wa SUMATRA,kunaendana sambamba na
kuombwa rushwa ambapo kama mtu hajatoa wanakamata basi na kuliweka kizuizini kwa muda mrefu bila
kushughulikiwa hali ambayo wanaona sijambo la kiungwana.
Kati ya mambo ambayo madereva hao wanalalamikia na
kupaza sauti zao ni swala la kunyanyaswa
na moja wa Afisa wa SUMATRA,ambapo wamesema nijipu linalo hitaji kutumbuliwa
mapema na Mh.Magufuli ambaye anaendana na Sera yake ya Hapa kazi tu nawao
wanafanya kazi ila hali inayowakumba nihiyo.
Mgomo huo huwaathiri
wananchi wanaotegemea usafiri huo hali inayofikia hatua kushindwa kufanya shughuli
zao za siku kutokana na mvutano huo na SUMATRA hali hiyo inawafanya hata
wanafunzi wanaoelekea shuleni kushindwa kufika kwa wakati nakurandaranda
kituoni hapo bila kujua hatima yao jambo ambalo bila kushughulikiwa halileti picha
nzuri kwa serikali hii ya awamu ya tano yenye kasi ya Hapa kazi tu na migogoro
ni mwiko.
Baadhi ya viongozi wa Chama cha Madereva Mkoani
morogoro jana wameelezea sababu za mgomo
huo kwa kina nakusema kuwa hadi kufikia hatua hiyo nikutokana na utendaji mbovu
wa Afisa mfawidhi wa SUMATRA Mkoa wa Morogoro kukamata hovyo daladala na kisha
kuwatoza faini bila sababu za msingi hali ambayo inawafanya wao wajione hawana
haki yeyote.
Baada ya mgomo huo wa Madereva JANA kufukuta kwa Saa 9 ilimlazimu Mkuu wa wilaya
ya Morogoro Bwana.Muhingo Rweyemamu kukutana na Madereva hao ambapo alisema
kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya inawaomba warudishe magari Barabarani
kwaajili ya kutoa huduma ya usafiri kwa wananchi mpaka siku ya Juma tatu
watakapokutana tena kutatua kero zinazowakabili,jambo ambalo limengonga mwamba
na madereva hao kuendelea na mgomo wao kama kawaida.
0 comments:
Post a Comment