Takwimu rasmi za serikali zinaonesha idadi ya watu
wanaojiua nchini Marekani imepanda pakubwa.
Takwimu hizo kutoka kwa Kituo cha Taifa cha Takwimu
za Afya zinaonyesha viwango vya watu kujiua vimeongezeka kwa karibu asilimia 25
katika kipindi cha miaka 15 iliyopita.
Visa vya watu kujiua vimefikia kiwango cha juu
ambacho hakijawahi kushuhudiwa tangu miaka ya 1980.
Utafiti huo uliangazia watu wa jinsia zote na marika
yote.
Viwango vya wanawake kujiua ndivyo vilivyoongezeka
zaidi, vikipanda kwa asilimia 36 miongoni mwa wanawake wa umri wa makamo.
Visa vya wasichana wa umri wa kati ya miaka kumi na
14 vimeongezeka mara tatu katika kipindi hicho.
Wataalamu wanasema hili huenda limesababishwa na
matumizi ya mitandao ya kijamii pamoja na watu kudhalilishwa mtandaoni.
Visa vya watu kujiua miongoni mwa Wamarekani asilia
vilipanda zaidi, karibu asilimia 90, ingawa visa vya kujiua miongoni mwa wanaume
weusi vilishuka kiasi.
Profesa Robert D Putnam kutoka Chuo Kikuu cha
Harvard anasema ushahidi zaidi unapatikana ukionesha uhusiano baina ya
umaskini, kutamauka na hali ya afya.
0 comments:
Post a Comment