Mkuu mpya wa Wilaya kinondoni Ali Salum Hapi
ameapishwa huku akitangaza wazi vita dhidi ya watumishi wazembe na wale wanaojihusisha
na ubadhilifu wa mali za Umma nakusema sasa yafaa wajiondoe wenyewe kabla
hajaanza kuwashughulikia kwani hahitaji watu wa namna hiyo.
Kauli hiyo ameizungumza wakati alipoapishwa jana na Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuwa mkuu wa wilaya ya kinondoni ambaye
aliteuliwa hivi karibuni na Rais Dr.John Magufuri na kuchukua nafasi ya Bw,Makonda ambaye aliteuliwa kuwa mkuu wa
mkoa wa DSM ambapo alisema wazi tu bila kumumunya maneno kuwa kasi ya
kuwashughulikia watumishi wasio waadilifu na wabadhilifu iliyoanzishwa na DR.Magufuri
na wasaidizi wake ataiendeleza kwa kasi kubwa katika wilaya hiyo.
Bw.Hapi amewataka watumishi wa wilaya hiyo kufanya
kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi zao huku kiupaumbele kikiwa kusikiliza na
kushughulikia kero za wananchi na Si Vinginevyo.
Mkuu wa Mkoa wa dsm akizungumza kabla ya kuapishwa
kwa bw,Hapi ametowataka watumishi wa idara pamoja na watumishi wa Umma katika
mkoa wa dsm kuahakikisha wanajiepusha na vitendo vya rushwa,ufisadi na Ubadhilifu
na kuapa kuwa hatosita kuchukua hatua kali dhidi yao.
Akizungumzia Uchunguzi unaoendelea wa kuwabaini
watumishi hewa amesema tayari wamebainika wengine 71 huku akiwataka wakuu wa
wilaya kuchunguza kila idara ili kuwabaini watumishi hewa na wakuu wa idara
husika amewatangazia kuwachukulia hatua mara moja pindi akibaini kuwa walitoa
taarifa za uongo dhidi ya watumishi hewa.
0 comments:
Post a Comment