Takriban
watu 17 kati ya 600 waliochukuliwa vipimo vya magonjwa yasiyopewa
kipaumbele wilayani Chunya katika mkoa wa Mbeya wameonekana kuwa na
vimelea vya ugonjwa wa vikope.
Dk Stanphod Mwakatage ndiye Mganga
Mkuu wa Wilaya ya Chunya amesema haya kwenye kijiji cha Saza wakati wa
Kampeni za Uzinduzi wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele nchini na duniani
kote, anasema katika utafiti uliofanyika mwaka 2013 kwa Halmashauri
11 nchini, Wilaya ya Chunya ilionekana kuwa na asilimia 3 ya watu wenye
vimelea vya ugonjwa wa vikope na hivyo kuwaomba wananchi kujitokeza
kumeza dawa ili kutokomeza magonjwa hayo.
Aidha Mratibu wa Magonjwa
yasiyopewa kipaumbele katika Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Merick
Mgonga amesema watu laki mbili,wanataraji kunywa dawa za magonjwa
yasiyopewa kipaumbele, lakini akadai kuwa zoezi hilo linakabiliwa na
changamoto ya ufinyu wa bajeti ,na ujazaji wa vitabu vya kumbukumbu.Source:Channel Ten.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment