MAMLAKA
ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa hadhari ya kunyesha kwa mvua
kubwa kuanzia kesho hadi mwisho wa mwezi huu, itakayosabaishwa na
kimbunga kiitwacho Fantala.
Kimbunga hicho kipo katika eneo la Bahari
ya Hindi kikienda kwa mwendo wa pole pole na kilikuwa hakijaleta
madhara, lakini kwa sasa athari zake zimeanza kuonekana.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi
alisema wanatarajia kuanzia kesho hali ya mvua itaendelea kuongezeka
katika maeneo ya Ziwa Victoria na maeneo ya Magharibi.
Alisema
kutokana na upepo kuvutwa na kimbunga hicho kwenda baharini, eneo kubwa
la nchi litakuwa na mvua kubwa hivyo, wananchi wametakiwa kuchukua
hadhari “Sasa tuko katika msimu wa mvua za masika, lakini kimbunga hiki
kitasababisha ongezeko la mvua, hivyo ni vizuri tahadhari
zikachukuliwa,” alisema.
Alisema tatizo kubwa la kimbunga hicho ni
mgandamizo mdogo wa hewa unaoweza kuvuta upepo kutoka maeneo mbalimbali
kwenda sehemu ambazo kimbunga kipo. Dk Kijazi aliongeza kuwa, kila siku
wakati wa kutoa utabiri, watatoa tahadhari ya maeneo yatakayoathirika
zaidi hivyo wananchi wanapaswa kuzingatia utabiri wa kila siku.
Alisema
vimbunga vimekuwa vikipewa majina na nchi zilizo Ukanda wa Pwani ambayo
hupendekeza kwa kufuata mpangilio wa herufi kulingana na msimu unaoanza
Novemba mpaka Aprili na hiki ni kimbunga ni cha sita, lakini siyo vyote
vyenye madhara kwa nchi.
Alisema vingine havijasikika kutokana na
kutokuwa na madhara kwa nchi, lakini Fantala kina madhara ya kusababisha
kuongezeka kwa mvua katika maeneo mengi ya nchi.
“Mpaka sasa tupo
kwenye msimu wa mvua za masika zinazoendelea kunyesha na kuna dalili
zinazoonesha kimbunga hicho kimeanza kuleta athari lakini kuanzia
Jumapili na mvua zitaongezeka zaidi,” alisisitiza.
Home
News
Slider
Mvua kubwa kuanzia kesho hadi mwisho wa mwezi huu,itakayosabaishwa na kimbunga kiitwacho Fantala.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment