Pia imewakamata waagizaji na wasambazaji wakubwa 24
wa bidhaa hizo wanaodaiwa pia kuwa wanahifadhi bidhaa zao katika majengo hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamata
shehena hiyo, Meneja wa Kanda ya Mashariki wa TFDA, Emmanuel Alphonce, alisema
msako huo ulianza juzi na kufanikiwa kukamata jengo moja la ghorofa tatu huku
mbili zikiwa zimejaa vipodozi vilivyopigwa marufuku.
Alisema baada ya kukamata jengo hilo walipata
taarifa kuwa kuna jengo jingine linalohifadhi vipodozi ambavyo vingi ni
vilivyopigwa marufuku.
“Leo (jana) tumekamata jengo jingine lenye ghorofa
tatu ambalo pia ghorofa zote zilikuwa na vipodozi ambavyo vingi ni vilivyopigwa
marufuku,” alisema Alphonce.
Alisema TFDA itaendelea na msako ili kuhakikisha
kuwa bidhaa zote zilizopigwa marufuku haziingizwi nchini.
Akizungumzia sakata hilo, Mkuu wa Kituo cha Polisi
Msimbazi, Saeda Elisha, alisema muda umefika wa kuwakamata wafanyabiashara
wakubwa wanaoingiza bidhaa zilizopigwa marufuku.
0 comments:
Post a Comment