Baadhi ya wanenguaji wa Papa wemba wakionekana hapa na nyuma ikionekana picha Ya marehemu Papa Wemba enzi za uhai wake.
Baadhi ya vijana na wapenzi wa Muziki wa Marehemu Papa Wemba wakionekana kujichora maandishi na Picha kwenye miili yao zikimuonesha Marehemu Papa Wemba ikiwa ni sehemu ya kumuenzi.
MWILI wa mwimbaji nguli wa muziki wa dansi nchini DR
Congo,Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba (Papa Wemba), umekwisha wasili nchini
humo ukitokea jijini Abidjan nchini Ivory Coast alipofariki mwishoni mwa wiki
iliyopita.
Msanii huyo alipoteza fahamu akiwa jukwaani alipokuwa
akitumbuiza mamia ya mashabiki na kuanguka na kukimbizwa hospitali na kufariki
dunia.
Mwili wa msanii huyo tayari umewasili nchini kwao na
kupokelewa na idadi kubwa ya watu katika uwanja wa ndege wa Kinshasa.
Wengi wao walionekana wakiwa wamevaa nguo zenye picha yake
huku zikiwa zimeandikwa ‘Kwaheri Papa Wemba’.
Gwiji huyo wa muziki wa lingala alizaliwa mnamo Juni 14
mwaka 1949, katika eneo la Lubefu - Wilaya ya Sankuru nchini Congo.
Alikuwa maarufu katika micharazo ya muziki wa Soukous,
alikuwa mmoja kati ya wanamuziki maarufu sana barani Afrika na kote duniani na
mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni haswa pale aimbapo akiwa jukwaani.
Papa Wemba, kama alivyofahamika na mashabiki wake, alikuwa
na umri wa miaka 66 na alikuwa amepata uraia wa Ubelgiji.
Vibao vyake ni kama Mwasi,show me the way, Yolele,
Mama,Proclamation"Chouchouna" (Papa Wemba), "Eluzam" na
" Mbeya Mbeya" (Evoloko Lay Lay), "BP ya Munu" (Efonge
Gina), "Mwana Wabi" , "Mizou" (Bimi Ombale) ,
"Zania" (Mavuela Somo.
Mwili wake unatarajiwa kupumzishwa katika makazi yake ya
milele Jumanne ya wiki ijayo mara baada ya kuagwa siku ya Jumatatu.
0 comments:
Post a Comment