Aliyekuwa
Kamishna wa TRA, Harry Kitilya, Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa
mwandamizi wa benki ya Stanbic tawi la Tanzania pia ni mshindi wa taji
la Miss Tanzania 1996, Shose Sinare April 27 2016 walikosa dhamana
kutokana na upande wa Jamhuri kukata rufaa mahakama kuu kupinga maamuzi
ya kupewa dhamana.
Leo April 29 2016 kesi hiyo ilitajwa kusikilizwa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam ambapo awali Hakimu
Mchauru alitoa maamuzi ya kuahirishwa kwa kesi hiyo mpaka Mei 12 mwaka
huu, sababu ni kutokana na jalada halisi la kesi kupelekwa mahakama kuu
baada ya kukatwa kwa rufaa ya kufutiwa shitaka namba nane la
utakatishaji fedha.
Muda mfupi baadae majira ya saa 4;30 asubuhi
walirudishwa tena mbele ya Hakimu Mchauru baada ya kupata amri kutoka
kwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam akitamka kesi hiyo
itajwe Mei 3 mwaka huu badala ya mei 12, aliyoipanga awali.
Hakimu
Mchauru amesema sababu za kupewa amri hiyo hazijui, hivyo kesi itatajwa
tena Mei 3 mwaka huu na yale yaliyozungumzwa asubuhi yatabaki kama
ilivyo, watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.
Home
News
Slider
Aliyekuwa kamishna ( TRA ) Harry Kitilya na wenzake warudishwa tena rumande mpaka Mei 3.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment