Watu
watano wamefariki dunia na wengine zaidi ya 13,933 kuathiriwa na
mafuriko katika wilaya za Kilosa, Kilombero na Malinyi kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha mkoani Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk.
Kebwe Stephen Kebwe amesema tathmini hiyo imetokana na mvua hizo
zinazoendelea kunyesha ambapo athari nyingi zimejitokeza ikiwemo vifo,
kuharibika kwa miundombinu ikiwemo barabara na madaraja pamoja na
kuharibika kwa nyumba nyingi za wananchi pamoja na mashamba.
Amezitaja
wilaya zilizoathirika zaidi ni Kilosa inayoongoza, Morogoro, Kilombero
na malinyi ambapo jumla ya waliopoteza maisha ni wa 5,mashamba yaliyo
haribika ni 12,073 nyumba 315 zimeharibika na wakazi zaidi ya 13,933
wameathirika katika kaya 3,095 kwa kukosa mahali pa kuishi na kulazimika
kupata hifadhi katika maeneo ya umma na kwa ndugu,jamaa na marafiki.
Hata
hivyo mbali na tathmini hiyo mkuu huyo amebainisha sababu kubwa
zilizosababisha kutokea kwa mafuriko katika maeneo mengi ikiwemo katika
kata ya Tindiga Manzese na msowero ni shughuli za kibinadamu ikiwemo
kilimo katika maeneo ya kingo za mto mkondoa, mto Miyombo na mto Msowero
hivyo kusababisha mito hiyo kujaa michanga na maji kuingia katika
makazi ya watu.
Home
News
Slider
Mafuriko yauwa watu watano na wengine zaidi ya 13,933 kuathiriwa wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment