Meya
wa Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam Mstahiki Boniface Jacob
amechukua uamuzi leo wa kufuta umiliki wa vizimba na vibanda takribani
miamoja vilivyokuwa vikimilikiwa na Watendaji pamoja na Madiwani wa
Manispaa ya Kinondoni kwenye soko la Mawasiliano la Simu 2000 na
kuagiza wananchi wapewe bure wafanyie biashara zao.
Mstahiki Jacob
aliyefuatana na watendaji wa Manispaa hiyo alitembea kwa miguu akiongea
na wamachinga mmoja mmoja na makundi kuanzia Ubungo Plaza hadi Ubungo
maji akiwaelimisha umuhimu wa oparesheni ya kuwaonda barabarani ikiwa ni
sehemu ya maandalizi ya ujenzi wa njia za juu na kuanza kwa usafiri wa
mabasi ya kasi Dart ambao hali ilibadilika pale alipotaja Manispaa kuwa
na masoko 26 yaliyohodhiwa na viongozi kwa kuingia Mikataba ya
kupangisha wakati wamejiagawia bure.
Aidha Mstahiki Meya Boniface
Jacob amesema katika kuhakikisha wafanya biashara wadogo wanatengewa
maneo yao watafanya uhakiki katika masoko yote kubaini viongozi na
watendaji waliojimilikisha na kuwanyang’anya ili masoko yatumiwe na
walengwa ikiwa ni hatua ya kuboresha mazingira ya jiji huku mtendaji wa
kata ya ubungo Bw. Gilbati Mushi akieleza hatua hiyo kudhirisha utawala
bora.
Home
News
Slider
Meya wa Kinondoni afuta umiliki wa vizimba 100 kwenye soko la Mawasiliano la Simu 2000.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment