Maafisa wakuu nchini Marekani wanasema kuwa Rais
Barack Obama atatuma wanajeshi ya ziada wapatao 250 nchini Syria, ili kuunga
mkono jitihada zinazofanywa na vikosi vya ndani vya nchi hiyo, katika kupambana
na wapiganaji wa Islamic State.
Kwa mujibu hao wa maafisa wa Marekani, lengo hasa ni
kuwasajili waarabu wa dhehebu la Sunni kuungana na wapiganaji wa kikurdi
waliopo kaskazini mashariki mwa Syria.
Hata hivyo vikosi hivyo vya Marekani havitawajibika
moja kwa moja katika mapambano hayo.
0 comments:
Post a Comment