Kiongozi wa mashtaka nchini Argentina ameomba idhini
ya mahakama kuanzisha uchunguzi katika shughuli za aliyekuwa rais wa taifa
hilo, Cristina Fernandes de Kirchner, juu ya madai kuwa alishiriki katika
utakasaji wa pesa haramu.
Uamuzi huo unafuatia ushahidi uliotolewa mahakama
Ijumaa na mfanya biashara, Leonardo Farina mshirika wake yeye na mumewe ambaye
pia alikuwa ni rais wa Argentina bwanaNestor Kirchner .
Akitoa ushahidi baada ya kuahidiwa kusamehewa makosa
yake mfanyabiashara huyo alisema kuwa Bi Fernandez na marehemu mumewe Nestor
Kirchner walishiriki katika shughuli kadhaa ya ulaghai wa fedha za umma.
Mfanyabiashara mwingine ambaye pia ni mwandani wa
familia ya Kirchner, Lazare Baez, alitiwa mbaroni mapema juma lililopita na
kulaumiwa kwa ulaghai wa Dola Milioni tano.
0 comments:
Post a Comment