Na.Devotha
Songorwa,Morogoro.
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia Mwanamume
Mmoja aitwaye SATOTI MAHENGE kwa kosa la Unyang’anyi kwa kutumia Silaha katika
kijiji cha Dodoma Tarafa ya Mlali wilayani Mvomero Mkoani Morogoro.
Mtuhumiwa huyo umri (33) ambaye ni mkazi wa Mafinga
Mkoani iringa pamoja na wenzake watano ambao hawajafahamika mara moja walitega gogo katika barabara kuu ya Iringa
Morogoro na kusimamisha gari lenye namba za usajili T,372 DCL MITSUBISHI CANTER
na kufanikiwa kupora simu 5 na fedha Taslimu 310000 na kisha kuwajeruhi watu 4 ambao walikuwa ndani gari hilo ambapo
mpaka sasa wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja.
Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro URICH MATEI amebainisha
hayo Mbele ya waandishi wa habari na kusema kuwa mtuhumiwa huyo wanamshikilia
zaidi kwa uchunguzi kusudi pia kuweza kupata jopo zima la watu aliokuwa
akishirikiana nao.
Kwa upande mwingine pia kamanda MATEI ameongeza kuwa
wanamshikilia mtuhumiwa mmoja anayefahamika kwa jina la BERNARD AMON,miaka 30,
mkazi wa Mawezi mlinzi wa kampuni ya QUICK SECURITY ambapo anatuhumiwa kwa
kufyatua risasi kwa uzembe na kusababisha majeraha kwa watu 2 ambao ni
RAMADHANI JAMES Miaka 21,mkazi wa Nanenane Oilcom na HUSSEIN ALLY,miaka 27
,mkazi wa kilakala ambaye alijeruhiwa mguu wa kushoto.
Hatahivyo kamanda MATEI amesema kuwa watuhumiwa wote
wapo mikononi mwa polisi na wanaendelea kuhojiwa na hatua kali za kisheria zitachukuliwa
dhidi yao.


0 comments:
Post a Comment