Licha ya Serikali kupaza sauti juu ya wananchi kuwa
na tabia yakuwa wasafi sehemu wanazo ishi lakini hali bado inaonekana
kujitokeza kuwa tofauti ambapobaadhi ya wakazi wa wilaya ya Handeni hatarini
Mkoani Tanga Afya zao zipo hatarini baada ya kunywa maji yanayotokana na
vinyesi vya binadamu.
Inaelezwa kuwa hadi kufikia hatua hiyo ni kutokana
na wananchi wa kukaidi maagizo ya kuchimba vyoo na hivyo kujisaidia Pembezoni
mwa Bwawa lililopo mji wa Chanika Wilayani humo lenye maji yanayotumiwa na
sehemu kubwa ya wakazi wake kisha vinyesi vyake hutiririka wakati mvua
ikinyesha na wananchi kuchota na kuyatumia bila kuchemsha.
Mganga mkuu wa wilaya ya Handeni Dr,CrediaNus Mgimba
amesikitishwa na kitendo cha wakazi hao kutumia maji ya vinyesi na kuwataka
kuacha mara moja kutumia maji hayo yenye vinyesi na wasio yachemsha na kuwataka
wakulima wanaolima pembeni mwa bwawa hilo nao kuacha kutumia eneo hilo
kujisaidia ili kudhibiti milipuko ya ugonjwa ya kipindupindu.
Wakazi wa eneo hilo wamekiri wazi kuwa maji hayo si
salama kiafya na hivyo kuiomba serikali kuweza kuwaboreshea miundo msingi
kwenye bwawa hilo ili kuzuia mtiririko wa vinyesi vinavyokwenda katika maji ili
kunusuru afya zao.
Kwaupande wake Mkuu wa wilaya ya Handeni Husna Msangi
amewataka wananchi kuzingatia kanuni za afya ili kuepukana na magonjwa ya
milipuko ikiwa ni pamoja na kuchimba vyoo,kuchemsha maji ya kunywa,kunawa
mikono na sabuni.


0 comments:
Post a Comment