Polisi nchini Kenya imewakamata vijana 17 wenye umri
wa miaka 12 hadi 26 katika mji wa pwani wa Mombasa ambao wamekuwa tishio kwa
wakazi na kufanya ujambazi.
Naibu kamishna wa Kaunti ya Mombasa Salim Mahmud
amesema, watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani leo kwa mashtaka ya kumiliki
dawa za kulevya na kujaribu kufanya uhalifu.
Habari zinasema, vijana hao ni wafuasi wa makundi ya
Wakali Kwanza na Wakali Wao yanayosemekana kuwa na uhusiano na mbunge wa huko
ambaye kwa sasa anachunguzwa kwa tuhuma za kuyafadhili..


0 comments:
Post a Comment