Polisi katika mji wa Chicago nchini Marekani
wamejawa na ubaguzi wa rangi, imesema ripoti mpya rasmi.
Ripoti hiyo imetayarishwa na jopo maalum lililoundwa
kutokana na ghadhabu ya umma baada ya polisi kulaumiwa kwa kuwapiga risasi
kiholela raia wasio Wazungu.
Jopo hilo limesema polisi waliwalenga watu weusi na
jamii ya Latino na hutumia nguvu kupita kiasi kukabiliana nao.
Ripoti hii imependekeza mageuzi 100.
Asilimia 74 ya mamia ya watu waliouawa na maafisa wa
polisi walikuwa raia weusi, licha ya kwamba idadi ya watu weusi ni asilimia 33
pekee.
Idara ya polisi mjini Chicago ndiyo ya tatu kwa
ukubwa nchini Marekani.
Aidha visa vya mauaji katika mji huo vilipanda kwa
asilimia 84 mwaka huu ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Kulizuka maandamano ya umma pale afisa wa polisi
Mzungu alipompiga risasi na kumuua kijana mweusi.
Maandamano hayo yalichochea Wizara ya Haki ya
Marekani kuanzisha uchunguzi dhidi ya mauaji hayo.
0 comments:
Post a Comment