Mgombea urais wa chama cha Republican nchini
Marekani Donald Trump amesema viongozi wa chama hicho hawataki ashinde uteuzi
wa chama hicho.
Akizungumza mjini New York, mfanyabiashara huyo
tajiri amesema Kamati ya Taifa ya Republican (RNC) inapanga njama dhidi yake.
Amesema hayo baada ya mpinzani wake Ted Cruz kupewa
wajumbe wote katika jimbo la Colorado licha ya kuwa upigaji kura haukufanywa
jimbo lote.
Bw Trump anaongoza kwa wajumbe katika kinyang’anyiro
cha kuteua mgombea urais wa chama hicho lakini huenda akashindwa kupata wajumbe
wa kumkabidhi ushindi wa moja kwa moja.
Hili huenda likapelekea kuwepo kwa mkutano wenye
ubishi Julai, wakati wa kuidhinisha mgombea.
Katika mkutano kama huo, wajumbe watakuwa huru baada
ya kura ya kwanza kupigwa kumuunga mkono mgombea yeyote.
Hili litafungua njia kwa Seneta wa Texas Bw Cruz au
hata John Kasich kuidhinishwa.
Gazeti la Washington Post liliandika Jumatano kwamba
Bw Cruz huenda akashinda kura ikipigwa mara ya pili kwa sababu amewashawishi
wajumbe wengi kumpigia kura hali kama hiyo ikitokea.
Lakini mwenyekiti wa RNC Reince Priebus amekana
madai ya Bw Trump kwamba sheria ilibadilishwa katika jimbo la Colorado kumnyima
wajumbe.
Bw Priebus ameandika kwenye Twitter kwamba utaratibu
wa uteuzi ulifahamika wazi kwa zaidi ya mwaka mmoja.
“Ni wajibu wa wanaofanya kampeni huufahamu.
Unalalamika sasa? Pole.”
Alipoulizwa katika mkutano mmoja katika mji wa New
Yrk iwapo kamati hiyo kuu inataka ashinde, Bw Trump alisema: “Hapana, sidhani.
Sidhani kamwe.”
Bw Trump ameshutumiwa kwa kutofanya kampeni za
kutosha katika majimbo kama vile Colorado.
Lakini Trump amesema wajumbe waliotaka kumuunga
mkono walitimuliwa na RNC.
"Hawanitaki kwa sababu natumia pesa zangu. Kwa
sababu hii ina maana kwamba hawawezi kunidhibiti kwa sababu nafanyia kazi
raia,” amesema.
0 comments:
Post a Comment