Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli amemteua Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe kuwa Balozi wa
Tanzania nchini Japan.
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 18 Aprili, 2016 na
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi wa Mheshimiwa
Chikawe umeanza tarehe 13 Aprili, 2016.
Kabla ya kupangiwa kituo hicho cha kazi, Mheshimiwa
Mathias Meinrad Chikawe aliteuliwa kuwa Balozi mnamo tarehe 15 Februari, 2016.
Mheshimiwa Chikawe aliwahi kuwa mbunge wa Jimbo la
Nachingwea kati ya Mwaka 2005 na 2015, na kwa vipindi tofauti katika serikali
ya awamu ya nne alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa nchi Ofisi ya
Rais Utawala Bora na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.


0 comments:
Post a Comment