Serikali
imesema bado ugonjwa wa malaria ni tatizo kubwa katika jamii hivyo
inafanya kila liwezekanalo kuhakisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo
yanaongezewa nguvu ili kuokoa watu wanopoteza maisha kutokana na
Malaria.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika hotuba iliyosomwa kwa niaba
yake na Mkurugenzi wa Huduma na Kinga katika wizarahiyo DK NEEMA RUTH
BEMAHILA wakati wa matembezi maalum ya kilomita tano ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya siku ya malaria duniani.
Katika maadahimisho hayo
kulizinduliwa filamu fupi ya namna ya kujikinga na ugonjwa wa malaria
ambayo itatumiwa kama moja ya nyenzo zitakazosaidia kuhimiza vita dhidi
ya malaria hapa nchini.
Nao waratibu wa matembezi hayo wamesema
mwitikio umekuwa mzuri na kwamba jambo muhimu ni serikali kuongeza nguvu
katika vita hivi kwani malaria inaepukika.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment