Klabu ya Simba SC ya jijini Dar es salaam
imethibitisha kushiriki michuano ya Kombe la Nile Basin Club Championship,
inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA)
itakayoanza kutumia vumbi Mei 22, 2016 nchini Sudan.
Mashindano ya vilabu Kombe la Nile Basin huandailiwa
na CECAFA kwa kushirikisha vilabu vilivyoshika nafasi ya tatu katika msimamo wa
Ligi kwa nchi wanachama wa CECAFA.
Bingwa michuano ya kombe hilo atajinyakulia zawadi
ya dola za kimarekani U$30,000, mshindi wa pili dola U$20,000, huku mshindi wa
tatu akipata kitita cha dola za kimarekani U$10,000.
Nile Basin inashirikisha vilabu kutoka katika nchi
wanachama wa CECAFA ambazo ni Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya, Sudan, Sudan
Kusini, Tanzania na Zanzibar.
Vitoria University kutoka Uganda ndio mabingwa
watetezi wa kombe hilo baada ya kuifunga AFC Leopards ya Kenya kwa mabao 2-1
katika mchezo wa fainali uliofanyika mwaka 2014.


0 comments:
Post a Comment