Timu ya Sevilla inaendelea kupambana kutinga fainali
za Uropa kwa mara ya tatu mfululizo baada ya jana kuibuka na ushindi wa penati
5-4 dhidi ya Athletic Bilbao na kutinga nusu fainali ya ligi ya Uropa.
Ilikuwa mchezaji Kevin Gameiro ndiye aliyefunga
penati iliyoamua matokeo ya mchezo huo baada ya penati nne za kila upande
kutinga wavuni huku kiungo wa Athletic Bilbao Benat akikosa penati.
Kwa ushindi huo ambao ulitokana na matokeo ya dakika
tisini ya michezo yote miwili kuwa mabao 3-3, Sevilla sasa inaungana na
Liverpool, Villarreal pamoja na Shakhtar Donetsk katika nusu fainali ya Ligi ya
Uropa.
Joto la mchezo lilipanda wakati wa kupiga matuta kiasi cha wachezaji kushikana mashati



0 comments:
Post a Comment