Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa
kuendelea wikiendi hii kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja mbalimbali
nchini, huku kila timu ikisaka ushindi katika michezo hiyo ili kujiweka katika
mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi.
Jumamosi, Young Africans watakua wenyeji wa Mtibwa
Sugar katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku Ndanda FC
wakiwakaribisha wakata miwa wa Kagera Sugar katika uwanja wa Nang’wanda Sijaona
mjini Mtwara.
Coastal Union watawakaribisha maafande wa JKT Ruvu
katika uwanja wa Mkwakwani jinini Tanga, huku Jumapili, Simba SC wakicheza
dhidi ya Toto Africans katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.


0 comments:
Post a Comment