Rais wa Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF), Jamal
Malinzi amempongeza Ravia Idarous kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Soka
Visiwani Zanzibar (ZFA) katika uchaguzi ulifanyika jana katika ukumbi wa Uwanja
wa Gombani, Pemba.
Katika salamu zake, Malinzi amesema anampongeza
Ravia kwa kuchaguliwa kwake, na hiyo imeonyesha imani kubwa kwa waliomchagua
kuongoza ZFA katika kipindi kingine.
Malinzi amewapongeza vingozi wote wapya
waliochaguliwa katika uchaguzi huo, na kuahidi kuendelea kushirikiana nao
katika shughuli zote za maendeleo ya mpira wa miguu.
Uchaguzi wa kupata viongozi wa ZFA ulifanyika jana
Gombani kisiwani Pemba, ambapo Ravia aliibuka mshindi na kutetea nafasi yake,
nafasi ya makamu wa rais Ugunja kienda kwa Mzee Zam Ali, na makamu wa Pemba
ikichukuliwa na Ali Mohamed Ali.


0 comments:
Post a Comment