Mhifadhi
Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dk Freddy Manongi amesema
Simba wanane na Tembo 25 wameuawa nje ya hifadhi hiyo kwa kipindi cha
mwaka jana kutokana na mauaji ya kulipiza visasi baina ya wananchi na
wanyamapori.
Akizungumza na wanahabari wakati wa ziara ya siku tano
yenye lengo la kuona athari za ujangili na juhudi zinazochukuliwa na
hifadhi hiyo kukomesha vitendo hivyo Dk Manongi amekiri kuwepo kwa
migogoro ya mipaka ambayo ipo karibu na makazi ya watu.
Amesema
tatizo la kuingiliana mipaka na hifadhi limekuwa sugu ambapo wakati
mwingine wanyama hao huingia vijijini kutokana na wanyama kutojua mipaka
huku akibainisha kuwa hivi sasa mamlaka hiyo imeimarisha ulinzi kwa
kuweka vituo vya Askari wa wanyamapori pori katika maeneo ya vijiji.
Hata
hivyo Dk. Manongi amesema ili kudumisha suala la ujirani mwema NCAA
inawekeza zaidi kwa wanavijiji vinavyozunguka hifadhi hiyo ambao hufanya
nao miradi mbalimbali ya maendeleo na kuwawezesha ili waione hifadhi
kuwa sehemu ya eneo lao.
Akizungumzia suala hilo Mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya ya karatu Mosses Mabula Amekiri kuwepo kwa
mwingiliano Kati ya wanayama pori na binadamu na kubainisha kwamba
ukinzani wa sheria ya wanyamapori iliyopo umekuwa ukichangia vitendo
hivyo kushamiri katika maeneo hayo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment