Wanawake
wajawazito na wanaojifungua hospitali ya halsmashauri ya wilaya ya Meru
Mkoani Arusha wameitaka halmashauri na serikali kutatua adha ya muda
mrefu ya akinamama wanaojifungua kunyonyesha kwa zamu vitandani.
Walitoa
kilio hicho muda mfupi baada ya hospitali hiyo kupokea msaada wa
vyandarua 446 vilivyotolewa kwa msaada wa wafanyakazi wa Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii tawi la Arusha kama sehemu ya kupambana na
ugonjwa hatari wa malaria.
Akipokea vyandarua hivyo Mganga Mkuu wa
halmashauri ya wilaya hiyo DR UKIO KOSIRIO amesema halmashauri hiyo
imefanikiwa kupunguza tatizo la malaria toka asilimia 30 hadi asilimia
tano.
Lakini hospitali hiyo imesema ilikuwa inakabiliwa na changamoto
ya damu na majengo ya wadi na sio vitanda peke yake ambavyo ndicho
chanzo cha msongamano wa kuwepo kwa malalamiko ya akinamama
waliojifungua kulalamikia adha hiyo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment