Ikiwa imepita siku moja tu kwa mitandao ya kijamii
kuonekana ikisambaa taarifa inayodai kwamba Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
ameyataka makampuni ya simu za mkononi kuzima data zao kila siku kuanzia saa
2.30 asubuhi mpaka saa 10.30 jioni ili kuzuia Watanzania kuwa online kipindi
cha muda wa kazi na masomo kwa wanafunzi taarifa hizo zakanushwa.
Taarifa hizo zimekanushwa na Ofisi ya Makamu wa Rais
na kusema kuwa Makamu wa Rais hahusiki na wala hajawahi kutoa agizo hilo hivyo Ofisi
hiyo inawataka watanzania kuwa makini na taarifa ambazo zinaibuliwa tu na watu
wasio julikana wakiwa na sababu zao kuzipuuza kwani taarifa hizo ni za uzushi.
Hata hivyo Ofisi hiyo ya Makamu wa Rais imetoa onyo
kali kwa watu wanaosambaza taarifa hizo za uzushi na kuwataka watanzania
kuwafichua watu wa namna hiyo wenye tabia ya kutoa taarifa za uongo kwa kutumia
jina la kiongozi huyo.
Pia Mheshimiwa Makamu wa Rais amewasihi watanzania
kutumia muda mwingi kuchapa kazi ili kujipatia maendeleo kwenye maisha yao na
siyo kutumia muda mwingi kufanya shughuli ambazo siyo za maendeleo kwa maisha
yao binafsi.
Aidha Serikali na vyombo vya usalama inaendelea
kuwasaka watu wanaochafua majina ya viongozi wakubwa wa nchi na watu wengine
kwa taarifa za uzushi na kuwachukulia hatua kali za Kisheria ikiwemo ile ya
Makosa ya Mtandao..


0 comments:
Post a Comment