Watu tisa wamekufa
na wengine zaidi ya mia saba
wamejeruhiwa baada ya kutokea tetemeko la ardhi katika kisiwa cha kyushu
kilichopo kusini mwa nchi ya japan.
Maafisa wamesema watu zaidi huenda bado wamenaswa
kwenye vifusi vya majengo yaliyoanguka huku maelfu wakikimbia makazi yao na
watu wengi wamekesha pembezoni mwa mji wa mashariki kwenye kisiwa hicho cha kyushu.
Waziri mkuu wa japan shinzo abe amesema kwa serikali
imetuma polisi, wazima moto na wanajeshi kuendesha operesheni za uokoaji na
kuwataka waliokumbwa na tukio hilo kuwa na subira wakati jitihada za serikali
za kuwaokoa zikiendelea.
Mpaka sasa hospitali nchini japan bado zinawapokea
waathirika wa tetemeko hilo kubwa la ardhi
lililokuwa na kipimo cha
richter 6.3 ambalo liliambatana na mengine madogo kadhaa.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kuwa
matetemeko hayo madogo yanaendelea licha ya kwamba baadhi ya watu wameamua kurejea hivyo hivyo katika
makazi yao kwa kuyaona hayatakuwa na madhara kwao.



0 comments:
Post a Comment