Nigeria imeelezea wasi wasi wake na mashaka ya
mkanda mpya wa video wa kikundi cha boko haram unaoonyesha picha za baadhi ya
wasichana wanaodaiwa kuwa wa shule ya chibok.
Mkanda huo unaonyesha picha za wasichana 15 waliovaa
mavazi meusi na bluu nyepesi wanaodaiwa kuwa ni miongoni mwa wasichana 276
waliotekwa miaka miwili iliyopita kwenye shule ya sekonari ya chibok.
Waziri wa habari wa nigeria bwana lai mohamed
amesema mpaka sasa serikali ya nchi yake
haina uhakika kwa asilimia mia moja kama wasichana hao ndiyo wale waliotekwa au
la.
Pia makundi ya watu ambao wamepotelewa na ndugu zao
wamekuwa wakikusanyika katika makundi makundi na kuanza kuziangalia sura
zinazoonekana kama ni za ndugu zao au la.
Katika maeneo mengine nchini humo maandamano yameendelea kufanyika kuishinikiza
serikali ya nchi hiyo kuongeza jitihada za kuwatafuta na kuwaokoa wasichana hao
ambapo hawajulikani walipo hadi sasa.
Kikundi cha kiislamu cha boko haramu kiliwateka
wasichana zaidi ya mia mbili miaka miwili iliyopita wakiwa shuleni na kutokomea
nao kusikojulikana ikiwa ni hatua ya kuishinikiza serikali ya nigeria
kutekeleza matakwa yao.
Matakwa hayo ni kutumika kwa sheria za kiislamu
katika baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo hasa katika mji wa maiduguri
kitu kilichopingwa na serikali na baadaye wakaanzisha harakati za kijeshi dhidi
ya serikali.


0 comments:
Post a Comment