Helikopta inayomilikiwa na jeshi la Afghanistan
imeripotiwa kuangushwa na kundi la Taliban katika eneo la milimani lililoko
mkoani Kunar.
Helikopta hiyo aina ya Mi-8 iliyoundwa nchini Urusi,
iliangushwa kwa kutumia bomu la mkono lililokuwa limetegwa ndani.
Bomu hilo lililotegwa lilianza kulipuka wakati
helikopta ilipokuwa ikijaribu kutua.
Kundi la Taliban limetoa maelezo na kudai kuwaua
wanajeshi wengi wa Afghanistan huku wengine wakiwachukuwa mateka baada ya
shambulizi hilo.
0 comments:
Post a Comment