Ikiwa ni siku ya kwanza ya Mkutano wa tatu wa Bunge
la kumi na moja kuanza huku bunge likitarajiwa kujadili na kupitisha bajeti ya
serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17 mjini
Dodoma baadhi ya wabunge wamelalamikia kitendo cha Serikali kufuta
Matangazo ya Bunge kutorushwa Mojakwamoja na Kituo cha Taifa (TBC)
Kwa hali ya kuoneshwa kukerwa na hali hiyo ya mfumo
mpya wa urushaji wa matangazo ya vipindi
vya Bunge wamesema kuwa wanavyoona nikuwa unalenga kuwanyima nafasi ya msingi wananchi
wanaofuatilia mambo na mwenendo wa Bunge ili kujua mwenendo wa wawakilishi
waliowachagua nivipi wanawasilisha matatizo yao ndani ya Bunge ili ya Tatuliwe.
Hivi leo Bunge limeoneshwa katika kipindi cha
Maswali na majibu kupitia Televisheni ya Taifa (TBC) Baada ya hapo yalikatwa na
utaratibu mpya ukaendelea.
Kwa nyakati tofauti tufauti baadhi ya wabunge wamedai mazingira ya
kuzuia vyombo vya habari vya Television kurusha matangazo hayo mpaka kupitia
kituo cha Bunge kuta kudumaza demokrasia na kuwanyima fursa wananchi kufahamu
uwezo wa wawakilishi wao.
Aidha akielezea Changamoto hiyo inavyoathiri
upinzani bungeni Mh.Peter Msingwa amesema vyama vya upinzania vitaendelea
kubadili mfumo wake kulingana na mazingira yaliyopo ili kukabiliana na hali
hiyo kwa lengo la kuleta uelewa kwa jamii.
Mhe Nape Nnauye mwenye dhamana baada ya kutafutwa kusudi
afafanue baadhi ya mambo yanayo lalamikiwa ili kutoa ufafanuzi wa changamoto
zinazojitokeza kutokana na Bunge kuamua kurusha matangazo ya vipindi vya Bunge
kwa kutumia studio zake amesema atajitahidi kukaa na wadau wa habari ili kuona
namna ya kulitatua suala hilo.
0 comments:
Post a Comment