Rais Dakta JOHN POMBE MAGUFULI amesema lengo la
serikali yake ni kutatua kero za wananchi na kwamba ingawa haziwezi
kuondolewa lakini amesema atahakikisha
kama siyo kuondolewa basi zinapunguzwa.
Rais MAGUFULI alikuwa akizungumza wakati wa ufunguzi
rasmi wa rasmi Daraja la Kigamboni lenye urefu wa mita 680 na barabara
unganishi upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa kilometa 2.5.
Kuhusu daraja la Kigamboni amesema linatarajia
kuraisisha usafiri na uchukuzi katika jiji la Dar es Salaam bila kutegemea
vivuko na vitu vingine vya uchukuzi ambavyo vimekuwa vikihatarisha usalama wa
watu.
Ujenzi wa daraja hilo uliogharimu shilingi bilioni
254 sehemu kubwa ya fedha zikitolewa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
NSF.
Rais Magufuli asema watakaopita daraja la Kigamboni
kuwa ni Bajaji,Baiskeli,Magari ambapo lazima walipie huku kwa upande wa
watembea kwa miguu wakipita bure kwa wakati huu wakisubiri hapo baadae kama
kukiwa na Mabadiliko ya kufanya nawao walipe.
Rais Magufuli amewataka watanzania kulitumia sasa
Daraja hilo la Kigamboni alilolizindua ili kuweza kujinasua kiuchumi.
Pia amesifu Watanzania kwa kufanikiwa kujenga
madaraja makubwa yakiwemo ya MKAPA,barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam kwenda
mikoa Kusini, Daraja la KIKWETE linalounganisha Kigoma na Kagera na Daraja la
Umoja linalounganisha Tanzania na Msumbiji.
Kwa upande wa daraja la Kigamboni amependekeza
liitwe Daraja la NYERERE kwa heshima ya Baba wa Taifa kwa kuthamini mchango
wake kwa taifa na pia alikuwa mtu wa kwanza kushauri ujenzi wa daraja la
Kigamboni.
0 comments:
Post a Comment