Ligi kuu ya Tanzania bara iliendelea tena mwisho wa
wiki kwa michezo mitano kupigwa.
Katika dimba la Taifa Jijini Dar Es Salaam klabu ya
soka ya Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Kagera Sugar.
Mabao ya wanajangwani hao yalifungwa na Donald
Ngoma, Amisi Tabwe na mlinzi wa kushoto haji Mwinyi akifunga bao la mwisho,huku
bao pekee la Kagera Sugar likifungwa na Mbaraka Yussuf.
Nao Azam Fc wakicheza ugenini kwenye dimba la
Kirumba huko Mkoani Mwanza walikwenda sare ya bao 1-1 na Toto Africans.
Matokeo ya michezo mingine ni
Stand United 2 – 0 Mgambo JKT
Ndanda FC 0 – 0 Tanzania Prisons
JKT Ruvu 1 – 0 African Sports
0 comments:
Post a Comment