Watu zaidi ya 100 wamekufa na wengine zaidi ya 200
wamejeruhiwa kutokana na moto uliozuka kwenye hekalu la wahindu nchini india.
Wengi wa waliojeruhiwa hali zao ni mbaya na
wanatibiwa kwenye hospitali ya chuo kikuu
katika mji wa Thiruvananthapuram,ambao ni mji mkuu wa jimbo la Kerala.
Moto huo umezuka leo alfajiri na umenzia kwenye fataki zilizokuwa
zimehifadhiwa kwenye hekalu hilo linaloitwa Puttingal,kwenye mji wa pwani wa Paravur katika jimbo la Kerala .
Fataki hizo hizo zilikuwa zitumike kwenye sherehe za
mwaka mpya wa wahindu.
Maelfu ya watu walikuwemo kwenye hekalu hilo,wakati
mlipuko mkubwa uliposikika majira ya alfajiri na moto kuenea kwenye jengo hilo na watu wengi
kunaswa ndani.
Waziri mkuu wa india, narendra modi
amekwenda kwenye eneo la tukio kujionea hali halisi.
0 comments:
Post a Comment