Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Mhe,Raziki Pembe Juma kuwa Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Amali katika hafla ya kuapisha Baraza jipya la Mawaziri
iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu,(katikati) Katibu Mkuu Kiongozi
Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha Mawaziri na Manaibu
Mawaziri wa Wizara 13 za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Mawaziri
wasiokuwa na Wizara Maalum ambao pia ni Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi.
Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Ikulu mjini
Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa vyama na Serikali pamoja na
wananchi kadhaa ambapo miongoni mwa waliohudhuria ni Makamu wa Pili wa Rais
Balozi Seif Ali Idd, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, Spika wa
Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid.
Wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Said
Hassan Said, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji na Mkuu wa Mkoa wa Mjini
Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis. Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar
Khatib Abrahman Khatib pamoja na viongozi wa vikosi vya Ulinzi.
Walioapishwa katika hafla hiyo ni Waziri, Ofisi ya
Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Ussi Gavu, Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.
Haroun Ali Suleiman. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara
Maalum za SMZ Mhe. Haji Omar Kheri,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud Mohammed.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Khalid Salum
Mohammed, Waziri wa Afya Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Elimu na Mafunzo
ya Amali Mhe. Riziki Pembe Juma pamoja na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee,
Vijana, Wanawake na Watoto Mhe. Moudline Castico.
Wengine ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko
Mhe. Balozi Amina Salum Ali, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mhe.
Balozi Ali Abeid A. Karume. Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe.
Hamad Rashid Mohammed. Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Mhe.
Rashid Ali Juma na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mhe. Salama
Aboud Talib.
Kwa upande wa Manaibu Waziri ni Naibu Waziri wa
Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Khamis
Juma Maalim. Naibu Waziri wa Afya Mhe. Harusi Said Suleiman na Naibu Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri.
Wengine ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na
Usafirishaji Mhe. Mohammed Ahmed Salum. Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili,
Mifugo nan Uvuvi Mhe. Lulu Msham Abdulla, Naibu Waziri wa Habari, Utalii,
Utamaduni na Michezo Mhe. Bibi Choum Kombo Khamis na Naibu Waziri wa Ardhi,
Maji, Nishati na Mazingira Mhe. Juma Makungu Juma.
Aidha, Dk. Shein amewaapisha Wajumbe wa Baraza la
Mapinduzi na Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalum akiwemo Mhe. Said Soud Said
kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum pamoja
na Mhe. Juma Ali Khatib Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na
Wizara Maalum.
Kwa uwezo aliopewa chini ya Vifungu 42, 43,44 na 47
vya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Dk. Shein ameunda Wizara 13 za Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuwateua Mawaziri na Manaibu Mawaziri wa Wizara
hizo pamoja na Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalum na Wajumbe wa Baraza la
Mapinduzi.
0 comments:
Post a Comment