Baadhi ya abiria walazimika kupanda daladala za kawaida na kuachana na usafiri mabasi yanayokwenda haraka-DART- kutokana na changamoto ya foleni kubwa ya kukata tiketi kwenye vituo,kusubiri mabasi kwa muda mrefu pamoja na mabasi hayo kutosimama katika baadhi ya vituo.
Katika vituo mbalimbali vya mradi huo abiria hao wamelalamikia utaratibu wa tiketi za karatasi na tatizo la mtandao katika utambuzi wa tiketi hizo na kuchelewa kufika kwa wakati kwa mabasi hayo kunasababisha msongamano katika vituo.
Nao baadhi ya madereva wa daladala wamesema licha ya idadi ya abiria kushuka lakini wameendelea kupata abiria hususani wanaotokana Posta, Kariakoo kwenda Mbezi na kuiomba serikali kuacha usafiri huo kuendelea licha ya kuwepo kwa mabasi hayo.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa wakala wa usafiri wa mabasi yanayokwenda haraka-DART- Mhandisi Ronald Lwakatare amekiri kuwepo kwa changamoto ya msongamano wa abiria hususani wakati wa asubuhi na jioni kunakosababisha na tatizo la mtandao katika utoaji tiketi.
Home
News
Slider
Abiria wakacha usafiri wa mwendo kasi nakupanda daladala kutokana na foleni ya ukataji tiketi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment