Image
Image

CHANGAMOTO:Ujenzi wa barabara ya viwanda kuelekea kwa Mawaziri walalamikiwa kwakuto kukamilika.

Ujenzi wa barabara ya Mikocheni viwandani kuelekea katika nyumba za mawaziri jijini Dar es Salaam ambayo inapitika kwa tabu mnoo kutokana na Shimo kubwa lililochimbika na maji kutuama hali ambayo imefanya watumiaji wenye magari yao wanaopita eneo hilo kupata tabu ya kupia.
Wananchi na watumiaji wa barabara hiyo waliozungumza na Tambarare Halisi mara baada ya kufika eneo hilo kujione namna barabara hiyo ilivyo wamepaza sauti zao kutaka kuweza kukamilishwa kwa barabara hiyo ambayo imechukua muda mrefu bila kukamilika kwake hali waliyoweza kusema hilo nijipu linafaa kutizamwa.
Wanasema tangia mwaka jana zoezi la kutengeneza barabara hiyo lilianza hali iliyofikia hatua inaenda kwa kasi kweli nakuamini kuwa huenda ingekuwa imekwisha lakini kumbe kilikuwa kama kiini macho kutokana na kipindi cha mwaka jana ndipo zilikuwapo harakati za uchaguzi za wagombea na viongozi kuomba kura kwa wananchi na kutoa ahadi kemkem kusudi waweze kuaminiwa na kupewa ridhaa ambapo baada ya hapo hadi sasa ujenzi umekuwa ni wakusuasua jambo linalo washangaza.
Wananchi hao wamewaomba  viongozi wenye dhamana kuhakikisha kuwa wanalifuatilia kwakina suala hilo ilikujua nini kinachokwamisha ujenzi huo kuto kukamilika kwa wakati,kwani wanaamini Serikali ya awamu ya tano nisikivu na haitaki masihara inataka watu wafanye kazi hivyo nawaliopewa kazi hiyo ya barabara wakamilishe. 
Hata hivyo Wamesema kuwa wakati ujenzi huo ukianza mwaka jana uongozi wa Manispaa ya Kinondoni ulisema kuwa fedha zipo zilizotengwa kwa ajili ya barabara za namna hiyo huku ukitoa ahadi za kutosha juu ya namna ya barabara hiyo itakamilika na ukatoa onyo kwa Madereva wa Malori yenye uzito mkubwa kupita katika barabara hiyo pindi itakapokamilika, jambo ambalo limekuwa tofauti na uongozi huo ulichokuwa umekisema.
Ujenzi wa barabara ya Mikocheni viwandani kuelekea katika nyumba za Mawaziri umekuwa ukisimamiwa na kampuni ya ukandarasi wa barabara ya Canopies toka mwaka jana,Juhudi za kuwatafuta kwa sasa tunaendelea nazo.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment