Mfanyabiashara maarufu wa mikoa ya Arusha na Singida,Jonathan Njamas amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela,baada ya kupatikana na hatia katika kosa la wizi wa mali ghafi ya kutengeneza vileo,yenye thamani ya shilingi milioni moja,mali ya kampuni ya Mega Trade Investment ya jijini Arusha
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya hakimu mkazi–Moshi,Joachim Tiganga amesema mfanyabishara huyo ametiwa hatiani kwa kosa la kuiga nembo ya kampuni ya Mega Trade Investment ya jijini Arusha inayotengeneza vileo aina ya Kiroba orginal.
Mfanyabishara huyo alikamatwa mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita,ambapo alikuwa anatafutwa kwa muda mrefu kutumikia kifungo hicho ambacho hukumu yake ilikuwa imeshatolewa wakati akiwa hayupo mahakamani.
Kesi hiyo ya jinai namba 186 ya mwaka 2012,ilifunguliwa na Jamuhuri katika Mahakama hiyo June 30 baada ya mshtakiwa huyo kukamatwa katika wilaya ya Moshi.
Home
News
Slider
Ahukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la wizi wa mali ghafi ya kutengeneza vileo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment