Abiria wa Kimara na Mbezi wakwama mwendo wa zaidi ya saa tatu katika vituo vya Mabasi ya Mwendo kasi wakisubiri abiria tokea Alfajiri ya 11 May 2016 jijini Dar es Salaam.
Hivi leo ikiwa ni siku ya pili ya mabasi ya mwendo kasi kuendelea kufanya majaribio ya kubeba abiria bure Hali ya Usafiri kwa Mabasi hayo imeonekana ya kusuasua hali ambayo imefanya abiria hao kukaa kwa muda mwingi kituoni hapo bila kujua hatma yao huku wengine wakisema pengine kwakuwa ni bure labda ndio sababu hawaji kwa wakati.
Katika kituo cha Kimara kinamama wenye watoto leo wameonekana kuwa waathirika wakubwa wa adha hii ya usafiri wa mabasi ya Mwendo wa kasi ambapo wameshauri kwamba muda nikitu cha muhimu sana hivyo nivyema muda ukazingatiwa kwani wao wanapata shida huku wakiwa na watoto, huku walikuwa wakiamini usafiri huo ungekuwa nafuu kwao kutokana na daladala kuwa zikijaza sana nawao kukosa nafasi ya kusafiri kwa wakati nakujikuta wakiwa kituoni kwa mwendo kasi.
Wamesema mradi huo utakapoanza kutoza pesa kwakila abiria huenda yakafanya kazi kwa wakati kwakuwa kila abiria atakuwa analipa pesa tofauti nasasa ambapo nibure, kwani walichokiona leo nikuwa mabasi hayo yanajiamulia muda wakuja pasipo kutambua kwamba wapo wanaoenda kazini.
Licha ya kupongeza huduma hiyo kuwa nzuri na yaharaka wamepaza sauti zao kuishauri Serikali na Mamlaka husika kuhakikisha kwamba mabasi hayo yanafika kwa muda vituo husika kubeba abiria badala ya kuchelewa huku kukiwa hakuna taarifa yeyote yenye kueleza sababu ninini ya kuchelewa ili kusudi kila mmoja ajue ninamna gani anatafuta usafiri na sikukaa kituoni tu.
Mabasi hayo ya Mwendo kasi yanatarajiwa kuanza shughuli za kubeba abiria kuanzia 12 May 2016, na abiria kulipa nauli kwa viwango vilivyoidhinishwa na Sumatra kwa maeneo husika huku wanafunzi nauli ikiwa nishilingi 200 tu.
Hii ndio Video ikiwaonesha abiria wa kimara wakipaza sauti zao leo.
0 comments:
Post a Comment