Image
Image

Rais Magufuli awasili nchini Uganda kushiriki tukio la kuapishwa Rais Mteule wa Uganda Yoweri Museveni.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais Mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati nyimbo za mataifa mawili pamoja na ule wa Afrika Mashariki ukipigwa katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na mwenyeji wake Rais Mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Maafisa mbalimbali waku wa vyombo vya  Ulinzi wa Serikali ya nchini Uganda mara baada ya kuwasili nchini humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika Ikulu nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima wakati akikagua gwaride rasmi la heshima mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kwenye kikundi cha ngoma za asili mara baada ya kuwasili kwenye Ikulu ya nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mwenyeji wake Rais Mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kwenye kikundi cha ngoma mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Entebe nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya maua kama ishara ya Ukaribisho kutoka kwa mtoto katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda mara baada ya kuwasili kutokea Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais Mteule wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati nyimbo za mataifa mawili pamoja na ule wa Afrika Mashariki ukipigwa katika Ikulu ya Entebe nchini Uganda.
Na.Mwandishi wetu,Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 11 Mei, 2016 amewasili Jijini Kampala nchini Uganda ambapo kesho anatarajiwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni.
Rais Magufuli ametua katika uwanja wa ndege wa Entebe majira ya saa tano za asubuhi na kupokelewa na Waziri wa Ujenzi na usafirishaji wa Uganda Mheshimiwa John Byabagambi na kisha kuelekea Ikulu ya Entebe ambako amepokelewa rasmi na mwenyeji wake Mheshimiwa Rais Yoweri Kaguta Museveni.
Akiwa katika Ikulu ya Entebe Rais Magufuli amekagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa heshima yake na pia amepigiwa mizinga 21.
Aidha, Viongozi hao wamefanya mazungumzo ambapo pamoja na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano na uhusiano kati ya nchi hizo mbili, Rais Magufuli amemhakikishia Rais Museveni kuwa Tanzania itatoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha ujenzi wa bomba la mafuta linalotarajiwa kujengwa kutoka Hoima katika Ziwa Albert nchini Uganda na kupita kaskazini mwa Tanzania hadi bandari ya Tanga.
Rais Magufuli ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mheshimiwa Suzan Kolimba.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment