Image
Image

Viongozi wa Madhehebu ya dini walaani mauaji ya viongozi watatu wa dini ya Kiislam waliouawa jijini Mwanza.

Viongozi wa dini wameitaka serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama kuhakikisha inawatafuta wahalifu wote waliofanya mauji ya kinyama katika moja ya Msikitini jijini Mwanza huku Baraza kuu la Bakwata likilaani mauaji hayo.
Akisoma tamko kwa niaba ya Baraza kuu la Waislamu nchini BAKWATA Shekh Mkuu wa Tanzania Shekh Abubakary Zubery Bin Ally ameonyesha kusikitishwa na tukio hilo na kusema serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi vinapaswa kuwabaini wahalifu na sheria kuchukua mkondo wake.
Aidha amesema tukio hilo lililotokea May 17 katika Msikitini wa Masjid Rahman mjini Mwanza wananchi na waislamu kwa ujumla hawanabudi kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za polisi wa kuwakata watuhumiwa wa tukio hilo.
Katika hatua nyingine Askofu wa Kanisa la Anglikan Dayosisi ya Dar es Salaam Dk Valentino Mokiwa akihutubia wakati wa ibada maalum ya kuadhimisha heshima ya mwanamke,iliyofanyika katika Kanisa la Anglikana ukonga amesema tukio la Mwanza halipaswi kujirudia.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment