Hospitali ya Rufaa ya Bugando inayohudumia mikoa ya Kanda ya Ziwa haina huduma ZA CT SCAN na MRI kwa muda wa zaidi ya miaka mitano baada ya zilizoko kuharibika tangu mwaka 2011 bila kufanyiwa matengenezo hadi sasa.
Daktari bingwa wa uchunguzi wa magonjwa kwa njia za mionzi katika hospitali ya Rufaa Bugando Dkt Godfrey Kasanga amesema mashine ya CT SCAN imefanya kazi wa muda wa miaka kumi na kuharibika.
Ukosefu wa vifaa tiba katika hospitali ya Rufaa Bugando ambayo inategemea vipimo vya CT SCAN katika hospitali za watu binafsi zenye gharama kubwa na kuisababishia serikali hasara ya shilingi milioni 270 kila mwaka kwa ajili ya vipimo vya watoto 600 wagonjwa wa mgongo wazi na vichwa vikubwa wanaotibiwa bure huku wengine zaidi ya 400 wakikosa huduma kutokana na ukosefu wa fedha za vipimo.
Zaidi ya shilingi bilioni tatu na milioni 400 zinahitajika kununua vifaa hivyo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment