Bunge limepitisha bajeti ya wizara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia, wazee na watoto, kwa mwaka 2016/2017 huku wabunge wakiitaka wizara hiyo kuhakikisha inatekeleza yale ambayo imeahidi katika bunge hilo kwa manufaa ya watanzania.
Wakichangia bajeti ya wizara hiyo, baadhi ya wabunge wamesema ni jambo la kusikitisha kuona vitendo vya unyanyasaji wa watoto na akinamama vikiendelea kukithiri nchini sambamba na kuangalia uwezekano wa masomo ya fani ya utabibu kutojirudiarudia.
Baadhi ya wabunge wamesema iwapo serikali itafanikiwa kutoa bima ya afya kwa wanawake wajawazito nchi nzima sambamba na kutekeleza kivitendo uboreshaji wa zahanati na vituo vya afya, afya ya mtanzania itaimarika.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment