Serikali ya Tanzania imetangaza Ijumaa kutenga dola milioni 20 kwa ajili ya kuanza mpango wa kukuza uchumi kiviwanda.
Waziri
wa viwanda na uwekezaji Charles Mwijage amesema serikali itaanza
utekelezaji wa miradi 18 ambayo inatarajiwa kuwezesha nchi hiyo kukuza
uchumi wake kutokana na viwanda hivi karibuni.
Waziri Mwijage
aliliambia bunge mjini Dodoma kwamba miradi itakayopewa kipaumbele ni
ile ya mkaa ya Liganga na Mchuchuma katika eneo la Njombe.
Miradi mingine ni ule wa magadi katika ziwa la Natron na kiwanda cha tairi cha Arusha.
Tanzania
inaendeleza sekta yake ya viwanda ili kutimiza ruwaza yake ya maendeleo
ya mwaka wa 2025 itakayowezesha nchi hiyo kuwa na uchumi wa wastani.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment