Image
Image

Fahamu kiundani chimbuko la Siku ya Mama' (Mother's Day) ya kila 8 Mei.

Utafiti umeonesha kwamba siku hii ya Mama' (Mother's Day)imeanza kutokana na sherehe za majira ya kuchipua (Spring) ya Wagiriki wa kale.
Sherehe hizo zilipendekezwa kwa mungu wa kike Rhea, mke wa Cronos, baba wa mungu.
Rome ya kale,kulikuwa na sherehe zilizofanana na hizi zilizopendekezwa kwa kumuabudu na kumpa heshima kubwa Sybil, mungu mwingine wa kike.
Hii imeanza takriban miaka 250 kabla ya kuzaliwa 'Iysa ('Alayhis-Salaam). Sherehe hizi za kidini za Warumi ziliitwa 'Hilaria' na zilidumu kwa muda wa siku tatu kuanzia Machi 15 hadi Machi18. 
Tarehe Za Kusherehekea Siku Hii Ya 'Mother's Day'Katika Nchi Mbali Mbali
Tarehe ya kusherehekea siku hii ni tofauti katika kila nchi na nchi.
 Norway wanasherehekea Jumapili ya pili katika mwezi wa Februari.
Argentina wao ni Jumapili ya pili katika mwezi wa Oktoba. Lebanon siku ya kwanza ya msimu wa majira ya kuchipua (spring).
Afrika Kusini ni Jumapili ya mwanzo katika mwezi wa Mei.
Ufaransa ni Jumapili ya mwisho ya mwezi wa Mei, wao hukusanyika katika chakula cha usiku kisha humpa mama keki.
Sweden huwa ni siku ya famiia Jumapili ya mwisho katika mwezi wa Mei.
Jamii ya Msalaba Mwekundu wa Sweden huuza maua katika plastiki ndogo ili wawape mama zao ambao wanabakia sikukuu kulea watoto wao.
Japan ni Jumapili ya pili katika mwezi wa Mei.
Amerika ya Kaskazini ambako hufanywa maonyesho ya picha za watoto wenye umri wa miaka 6-14.
Maonyesho hayo yanaitwa 'Mama Yangu'.
Kisha maonyesho hayo husogezwa kila baada ya miaka minne na kutokeza nchi mbali mbali.
Nchi nyingine nyingi husherehekea ziku hii kwa tarehe mbali mbali.
Nchi za Arabuni imeanza kusherehekewa Misri nayo ni tarehe 21 Machi 1956.
Siku hiyo pia ni siku ya mwaka mpya wa Wakristo Wa Kikhufti (Coptic Christians) na sherehe za Nawroz za Wakurdi.
Kisha tena ndio ikaenea nchi zote nyingine za kiarabu. Na wote hao walioanza kusherehekea sikukuu hii ni aidha washirikina, Mayahudi au Manaswara. 
 Kufahamu kwa kina zaidi na zaidi BofyaHapa:-http://bit.ly/1WhSWy3
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment